
Sahibu Adibu...................... na Kelvin K. Motuka Nyonda iliyojiotea aa, kwako nana mepevuka aaa Kumbe haikuotea aa, chechele ’kanyagika aaa Dume ninaitetea aa, kutua pa hakika aaa... (Ni huba zuri swahiba aaa, thamani ya milele eee) (Sifa bainifu muhibu uuu, adabu ya tukizi iii) Upo pema moyo wangu uu, laazizi wangu Floli iii Umeufungia pingu uu, katu sisonge mahali iii Naondokea uchungu uu, nikifurahia hali iii... Basi udumu twaomba aa, kielelezo cha kuigwa aaa Unyumba kila nyumba aa, iwe asasi furaha aaa Kizazi na kingine ee, tarjama waijue ee... Malenga wa Vilimani (Aprili 24, 2026)

