
HONGERA BI. RAELI! Umesikia kengele, kwamba saa imetimu Ni ishara kulichele, ushike njia mwalimu Japo wafika kilele, na kuondoka ndo zamu Bi Raeli Nyagesoa, twatamani ukawie Jamvi unalokunja, ingekuwa wakunjua Tajriba hawajaonja, walimu wanoingia Nyingi iwafae nyanja, wakipenda kupakua Na vikembe wafaidi, hekimayo Bi Raeli Lau ni uwezo wetu, saa tungeshikilia Beliring’a kukutu, mikonoye kukwamia Usalie huku kwetu, ujuzi kutupatia Tungeridhia utoke, tukishiba Bi. Raeli Akilini twakuona, utokapo kichwa juu Tunakuhongeza sana, japo kubwa tuna kiu Sauti yako mwanana, ya upole namba tuu Mengi imesuluhisha, mama yetu Bi. Raeli Tunakuaga kwaheri, tukiyashusha machozi Ikufate basi heri, jaza ujazwe mlezi Mema yako ni uturi, kwa vizazi na vizazi Ingawa wavua buti, tarjama itadumu Malenga wa VILIMANI (Kelvin Kombo Motuka) Februari 12, 2026

