Song Cover Image

Alivyokuumba by Kelvin K. M

Livokuumba Dayani Hili sasa naloghani metunga kabla Juni lako we hurulaini urembo wako kiini Lipokuona mwanzoni ningepata afkani livokuumba Dayani kukunyima walakini Zilivyoshuka herini ulimbwende so kifani nao utuvu usoni unokaa kusakini Masihara na utani sihusiki asilani ni nususi sijabuni wa kupinga hili nani Kufu yangu navyodhani umbo la nje hata ndani si sharti hadubini ili hilo kubaini Lipojiweka mizani nilihisi kitu duni nikanywea hadharani kadhalika faraghani Haweva mie sachani tenda hata mfundani kitilia akilini uwepo wake Manani Litaraji ushindani wajipange kwa foleni kataka kukupa cheni nyerezi iwe rubuni Ninyamaze haja gani kipata yako leseni nichukue usukani kuwa mie ndo rubani Napofika tamatini nione mie imani penginepo nilizini daima kukutamani Malenga wa Vilimani (Kelvin Kombo Motuka) Mei sita, twenti fiftini