
Ahsante Rais! Amri yako Rais Kwa wizara ya fedha Kadhalika ya elimu Imekuwa nusura yetu Walimu wote wa bodi Tuso na walau mtetezi Ahsante Rais! Ahsante Rais, wa bodi nao walimu Chozi lino lenye shari, mepisha chozi la heri Ahsante Rais, wa bodi nao walimu Imetuchoma miale, tukakosa na udole Madhila kenda kilele, tukadhani ya milele Ahsante Rais, wa bodi nao walimu Kilio ngawa kirefu, kumbe nacho kina mwisho Ilijitenga sarafu, tukangoja wiki kesho Imetujia insafu, tukapata uhuhisho Ahsante Rais, wa bodi nao walimu Kila likeupukalo, lina heri nawe, mja silalame Lolote lijaliwelo, lino mpaka liwe, vipi likuchome Ikawa liandikwalo, kudura ujuwe, hata wapi ukahame Aliloridhia ndilo, furaha tutuwe, gumu litukome Ahsante Rais, wa bodi nao walimu Kelvin Kombo Motuka Malenga wa Vilimani September 23 twenty twenty Nyamataro.

