
Mbele Daima......na Kelvin Kombo Motuka (Juni 4, 2026) Mbele daima! Wazidi kulonga, na kusonga misamba mikubwa zaidi kila siku. Mbele daima! Walonga kumbatia tija ya daima kutoenda mbele wakati muhimu zaidi. Mbele daima! Nasisitiza – mbele la! Uzidipo utamu, wakati mwingine iza Pinda, maradufu ongeza, hatua kinyumenyume Huo ni mwafaka mzuri kupindukia Ni dharura kutafakari Mbele daima! Nanena tena - mbele hasha! Nyuma daima Lau mto uvukao, kabla ya mkeka wa matamu Unazidi kuvimba Utamu huwa kileleni, ukaribiapo uchachu.

