
Nimeuchinja moyo! Watiririshia damu, maozi yake mapofu Hoi umo ndani humu, huna nguvu kwenda rafu Ndani mwake utadumu, kujitonesha una hofu Nimeuchinja moyo! Nimeutoa kafara, lengo uize harara Ujana una hasara, kwa moyo ulo imara Uuguapo madhara, ndani chuo yanagura Nimeuchinja moyo! Shabaha ufinyike, na akili ipanuke Sikongowee wa kike, na ashiki usishike Nachinja niimarike, nyanja nyingi niinuke Nimeuchinja moyo! Usivutwe na vitamu, na kujazika hanjamu Ufahamu zipo sumu, mionjo yake mitamu Upo ndani ni awamu, uzingatie muhimu Malenga wa Vilimani (Kelvin Kombo Motuka) Juni 29, 2026

