Song Cover Image

Mbona kutukwaza? (Kelvin K. M)

Kwani kutukwaza? Yule alipotugusa, nyinyi mlituunguza Akiwa atupangusa, duni mkatupunguza Hakutaka kutukweza, mlipo mkatukwaza? Akaanza kutukuza, mkatuombea kiza? Alipo tuimarisha, mkawa mwatumaliza Zawadi yake ya kasha, tusipate mkakaza Mkapenda tuwe bure, kila leo tule pure Alipotaka tung’are, mkatuonea gere Malenga wa Vilimani (Kelvin Kombo Motuka) Oktoba 3, 2024