
Nikande Nikande nithibitishe, sura unirejeshee Nikande nichangamshe, utulivu nipatie Nikande uniuhishe, wakulivu nondolee Nikande ni majeruhi, mahasidi wanivyoga Nikande Bwana nikande, nikande unipe tiba Nikande moyo sipinde, iniepuke taaba Nikande kisha nilinde, na hasidi waso toba Nikande ni majeruhi, mahasidi wanivyoga Nikande kishanitua, mzigo wa masimango Nikande kunisugua, mavune yenye ukongo Nikande kinivuvia, hasa moyo sio shingo Nikande ni majeruhi, mahasidi wanivyoga Nikande unitulize, kwa mawe ninorushiwa Nikande kisha nipoze, kwa fujo nashambuliwa Nikande uniliwaze, nihani moyo kutuwa Nikande ni majeruhi, mahasidi wanivyoga Nikande ukikusanya, vipande pamwe vya moyo Nikande ziba mianya, ukikaushe kiliyo Nikande wameniminya, wanadamu wenye choyo Nikande ni majeruhi, mahasidi wanivyoga Nikande nitabasamu, moyo utie viraka Nikande kwa mariamu, mwanao niimarika Nikande nina hamumu, mja nimeshasagika Nikande ni majeruhi, mahasidi wanivyoga KELVIN KOMBO MOTUKA (Malenga wa Vilimani) Agosti thati wani, twenti twenti wani

