NIKITOKA PATE! Yanikabili mavune, na shingo nimeipinda Nakujia unione, shambani nilivyoshinda Naja mradi nipone, makovu ukinikanda Ungekuwa na roshani, ungetoka kwangalia Ela songa dirishani, ulisogeze pazia Halafu huko njiani, tupa jicho chungulia Ninaipiga misamba, nimeyavuja majasho Yako yanivuta kamba, nitoke kwenye malisho Nikifika kama kimba, nitaanza kwenye josho Nijitingapo taulo, nije ndani kubarizi Naomba un'pime kilo, unipigishe mbizi Huno ndio wangu mlo, nishakiri niwe chizi Nitapita kotekote, na kukuangua nazi Nikishakutoka Pate, nitashika usingizi Nitulie ning'orote, kidarini kwa malazi Malenga wa Vilimani (Kelvin Kombo Motuka) Machi 10 2025