Saa yangu Sasa basi, nipe ridhaa niende Nende kasi, ya kutenda niyatende Bisibisi, nipe niende niunde Saa yangu imetimu! Imetimu, sitaki kulimatia Nina hamu, hima papo nikatua Na jukumu, langu kuwajibikia Wasaa wangu mefika! Maskani, tayari kaandaliwa Yenye feni, kwa nari nikavuviwa Asilani, tamaa sitoondowa! Wakati hasa ndo huu! Pitapita, zenye na kutolowea Kutonata, mkono nazipungia Naikata, miguu ya kutembea Kwani dakika ndo hii Ndiyo hii, kama siyo gani basi? Ndiyo hii, wondoka utusitusi Ndiyo hii, kuponyoka si rahisi Ndiyo hii saa yangu! Saa yangu, ndiyo saa yangu hasa Rabbi Mungu, katoe ridhaa sasa Wanguwangu, pangu nami kujitosa I hapa awamu yangu! KELVIN KOMBO MOTUKA (Malenga wa Vilimani) Shule ya Wasichana ya Nyakach. Julai kumi na sita, twenti twenti wani