
Njiwa peleka salamu, ooh kwa yule wangu muhimu x 2 Umweleze afahamu, kwamba ninapata tabu x 2 Hali yangu mahamumu, ooh maradhi yamenisibu x 2 Ewe njiwa ewe njiwa aaaa (Peleka salamu) Ooh Kwa yule kwa yule (wangu muhimu) x 2 Usiku kucha nakesha, ooh na yeye ndiye sababu x 2 Iwapo haji maisha, itamfika aibu x 2 Pendo langu halijesha, ooh ndilo linaniadhibu x 2 Ewe njiwa ewe njiwa aaa, (Peleka salamu) Ooh Kwa yule kwa yule (Wangu muhimu) x 2 Njiwa usihadaike, nenda ulete majibu x 2 Nenda upe-si ufike, mkimbilie swahibu x 2 Mbele yake utamke, ooh ni yeye wa kunitibu x 2 Ewe njiwa ewe njiwa aaa, (Peleka salamu) Ooh Kwa yule kwa yule (Wangu muhimu) x 2 Ukifika tafadhali, ooh sema naye taratibu x2 Ukisema kwa ukali, mambo utayaharibu x2 Kamwabie sina hali, ooh kufariki si ajabu x 2 Ewe njiwa ewe njiwa aaa, (Peleka salamu) Ooh Kwa yule (kwa yule wangu muhimu) x2

