
Hapi bathidei Poly, uishi umri tawili Julai ndo yetu wawili, mwezi wa baraka na utuli Upate tele bin Momanyi, ukwasi wa hali (Furahia ndugu yangu, baraka tele za Mungu Aliyekulinda tangu, yako akupe nzima chungu) 2 Polykap heri njema, furaha neema za Mungu Kila lako liwe jema, lijitenge nawe chungu Matatani uwe wima, baraka ziwe lako fungu Afanye Poly Giteya Uwe askari wa Yesu, kazi uifanye kwa haki Jema silifanye nusu nusu, ulifanye lisibaki Yakujie yalokuhusu, toka kwa Mgawa riziki Malenga wa Vilimani Kelvin Kombo Motuka Julai 3, 2024

