Hima naenda kitalu Linatoka ubichini, likapevuke waridi Lenda chanua majani, tamviri maridadi Lanionekea geni, hasha si lile la jadi Waridi n'taliatika, panapo yangu maozi Panapo yangu maozi, niliole nikitaka Halaiki wamaizi, ndilo langu la hakika La kunusa waziwazi, nekta kuliwazika Rihi yake inigande, ikawe kichomanguo Ikawe kichomanguo, kote initambulishe Moliwe lipe ridhio, waridi linawirishe Lipate afya kwa chuo, limee likawe sheshe Waridi liwe aula, moyo lipambe daima Moyo lipambe daima, nijisikie sukari Kitalu naenda hima, yangu nia sighairi Natumaini Karima, taidhini yangu ari Kabla jua kutua, chaa nataka kufika Kelvin Kombo Motuka (Malenga wa Vilimani)