
SAUTI KUU INANIITA ISAC KUCHA MBILI (ISAC 2K) [INTRO — SPOKEN RHYTHM] Sauti ya haki, inalia mitaani, Machozi ya watu, yanadondoka gizani. Si chuki, si kisasi, siyo tangazo la vita, Ni sauti ya ukweli, nimesikia, nimeitika! [CHORUS — GOSPEL] Sauti kuu inaniita, Nihubiri habari njema. Roho wa Bwana yu juu yangu, Amenitia mafuta. Niwahubirie maskini, Niwaambie habari njema. Wafungwa wafunguliwe, Vipofu waone tena. Waliosetwa waachiwe, Watoke vifungoni. Kutangaza mwaka wa Bwana, Uliokubaliwa! Sauti kuu inaniita, Niitetee haki! Nihubiri ukweli, Nikemee uovu! Nihimize uzalendo, Haki iwe kwa wote! Naam, Bwana, nimeitika! [VERSE 1] Katiba ni dira, si karatasi ya kitabuni, Madaraka ni dhamana, si tiketi ya kutawala. Bunge liwe na meno, Serikali iwajibke, Mahakama ihukumu, isimwogope kaizari. Mdude wa Mbeya, Mei mbili akatoweka, Julai tisa, ombi likakataliwa. Familia inamtafuta, majibu hayajafika, Mdude yuko wapi? Taifa linauliza! Polepole, Oktoba sita, taarifa ya kutekwa, Mlango umevunjwa, chini damu imetapakaa. Mama anaita mwana, majibu hayajafika, Humphrey yuko wapi? Ukweli ujulikane! Oktoba ishirini na tisa, vilio mitaani, Risasi, majeruhi, hofu hospitalini. Tume ikasema, mia tano kumi na nane, Mbeya themanini—hizi ni roho za nani? Mtandao ukazimwa, sauti zikazimwa, Familia na wagonjwa, mawasiliano yakaminywa. Polisi ni walinzi, ndo chanzo cha hofu, Nguvu ikivuka sheria, nani awajibike? [CHORUS] [VERSE 2 — UCHAGUZI NA MAHAKAMA] CHADEMA ikazuiwa, uchaguzi hadi ishirini thelathini, Ushindani ulikuwaje? Waulize wananchi! Mara Mpina kakatwa, maamuzi yakabadilika, Kura ya mwananchi, thamani yake ikabagazwa. Lissu nyuma ya nondo, Aprili ishirini na tano, Siku mia tano sabini na saba, haki bado gizani. Maamuzi ya ukakasi, wanazuoni wanadadisi, Kesi inatetewa,hukumu inatetewa,jaji anatetewa,na mahakama inatetewa?.. Novemba sita, uhaini ukatoka, La uchochezi likaibuka, hukumu ikatolewa. 623/2026 iwe namba ikawa namba ukombozi.. Miaka minne kwa uchochezi, rufaa inasubiri, Historia inaandika, wananchi wanadadisi. Sheria ina jicho moja tu, inamwona mpinzani tu,inamwona mkesefu tu,hata kabla hajawaza tu. Wahuni wanazura,na magari,wanahabari na kauli zenye hatari. Polisi haiwaoni,haiwagusi hao watoto wema,watakatifu,inawalinda. Mtekaji yuko mitaani, mtekwaji hatiani,kanuni za milele za maisha,zimegeuka? Ni usanifu mpya wa historia,nani atajibu mahakamani? DPP aseme wazi, ushahidi uwekwe wazi, Dhamana siyo hisani, kesi ipimwe kwa mizani ya sheria. Haki ikicheleweshwa, matumaini yanapotea, Muda unapozidi, familia zinateseka. Anayechunguza rushwa,naye anapokea rushwa,ili aichiunguze rushwa,mbele ya mla rushwa,kesi inarushwarusha,nipeni kitu cha arusha.... Mfungwa ni binadamu, heshima yake ionekane, Mtuhumiwa si mfungwa, mipaka yake ijulikane. Mahakama si mateka, iwe nguzo ya dola, Ushahidi uwe kipimo, si amri ya mtu wala! [CHORUS] [VERSE 3 ] Ardhi ni maisha, sikiliza wakulima, Mfugaji ana haki, asifukuzwe kimyakimya. Hazina si ya walafi, ni jasho la wananchi, Mikataba iwe wazi, tusifichiane gizani. Manunuzi ya umma, yawekwe wazi kwa jamii, Uteuzi uwe sifa, si undugu na ushkaji. Taasisi zisimame, ziwajibike kwa wananchi, Jeshi liheshimu mipaka, ya mamlaka za kiraia. Mtoa taarifa alindwe,kwetu anapewa kesi,fuvu la binadamu, kucha za simba na meno ya tembo. Kibongobongo akilindwa, kesi inageuka mchongo. Atawekwa ndani ya boxi,mahakama iwe komedi.. Mahakamani maigizo, haki inapigwa tobo tu? Serikali itoe majibu, inapovunja sheria, Uwajibikaji si kisasi, ndiyo msingi wa taifa. Uzalendo si kusifu, wala kufumbia macho, Kuipenda nchi ni kuuliza maswali magumu. Maendeleo bila haki,sawa na nyumba bila msingi. Sheria kwetu wote, tajiri na maskini. Madaraka siyo urithi, wala mali ya familia, Nchi ni ya wananchi,na haki iwe njia! [BRIDGE — SPOKEN WORD] Mathayo 5:20: “Haki yenu isipozidi ile ya waandishi wa sheria na Mafarisayo, hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.” Haki ianze kwangu! Haki ianze kwako! Haki ianze kwa viongozi! Sheria iwe kwa wote! [FINAL CHORUS ] Sauti kuu inaniita, Nihubiri habari njema. Roho wa Bwana yu juu yangu, Amenitia mafuta. Niwahubirie maskini, Niwaambie habari njema. Wafungwa wafunguliwe, Vipofu waone tena. Waliosetwa waachiwe, Watoke vifungoni. Kutangaza mwaka wa Bwana, Uliokubaliwa! Sauti kuu inaniita, Niitetee haki! Nihubiri ukweli, Nikemee uovu! Nihimize uzalendo, Haki iwe kwa wote! [OUTRO — SPOKEN WORD] Nani yuko juu ya sheria? Hakuna hata mmoja! Madaraka ni dhamana! Si umiliki! Sikutumwa kusifu madaraka, Nimetumwa kutetea haki! ISAC KUCHA MBILI (ISAC 2K)

