
Nitakuchosha Floli by Kelvin K. M
Nitakuchosha Nitakuchosha bibiye, wallahi nitakuchosha Nitakuchosha miye, kwa huba pia bashasha Nitakuchosha uliye, zitakuliza bahasha Nitakuchosha jameni, ukalemewe na nyonda (Niwe GOAT memsapu, kubanduliwa muhali, Floli Kem linda himaya Huba tulipige ripu, ling'ae nyonda Floli, tusiwe kama kaa haya) 2 Nitakuchosha ujuwe, kukuchosha sitochoka Nitakuchosha tu wewe, pako juwa sitotoka Nitakuchosha u’guwe, wadi yangu kulazika Nitakuchosha sichoke, nitakuchosha billahi (Niwe GOAT memsapu, kubanduliwa muhali, Floli Kem linda himaya Huba tulipige ripu, ling'ae nyonda Floli, tusiwe kama kaa haya) 2 Nitakuchosha kikweli, takuchosha memsapu Nitakuchosha kwa hili, hili na lile kwa kapu Nitakuchosha kihali, pangu sipate utupu Nitakuchosha swahiba, sio mwiba mapendevu (Niwe GOAT memsapu, kubanduliwa muhali, Floli Kem linda himaya Huba tulipige ripu, ling'ae nyonda Floli, tusiwe kama kaa haya) 2 Nitakuchosha matamu, sema kwani n’sikuchoshe Nitakuchosha salimu, amri nikakuchoshe Nitakuchosha karamu, kwa yote nikushibishe Nitakuchosha bibiye, mradi uwe u radhi (Niwe GOAT memsapu, kubanduliwa muhali, Floli Kem linda himaya Huba tulipige ripu, ling'ae nyonda Floli, tusiwe kama kaa haya) 2 Nitakuchosha uchoke, unyong’onyee kwa nyonda Nitakuchosha mwa’mke, azmani sitopinda Nitakuchosha lishike, matunzo mithili kinda Nitakuchosha we' peke , usichoke mamachanja (Niwe GOAT memsapu, kubanduliwa muhali, Floli Kem linda himaya Huba tulipige ripu, ling'ae nyonda Floli, tusiwe kama kaa haya) 2 Nitakuchosha kuchosha, jingine sina wallahi! Nitakuchosha bashasha, mpaka utoe siahi Nitakuchosha kinyesha, kipusa pia billahi! Nitakuchosha lazima, vinginevyo miye sina (Niwe GOAT memsapu, kubanduliwa muhali, Floli Kem linda himaya Huba tulipige ripu, ling'ae nyonda Floli, tusiwe kama kaa haya) 2 KELVIN KOMBO MOTUKA (Malenga wa Vilimani) Agosti Saba, twenti twenti wani

