
Naapa sikuati Nashindwa niseme nini, kwalo penzi la dhati Mahaba yaso kifani, kwangu sio katiti Hadi keshoye mwandani, naapa sikuati Sura sina shauku , vazi unyenyekevu Mpendi hino si chuku, umenipa utuvu Nangoja siku ya siku, nikuone laivu Nilijua ua zuri, tangu shule katulia Mejengeka yangu ari, ua kulikaribia Niuenjoi uturi, uua kufurahia Sitokufunga kifungo, huria nakuachia Nyingi nitatunga tungo, uzuriwe kusifia Sio kukuhonga hongo, ila haki kupatia Malenga wa Vilimani (Kelvin Kombo Motuka)

