Song Cover Image

Umechanika Moyo (Kelvin K. M)

Umetenda hukujali, Kwamba laniumiza hili, Ela siulizi swali, Langu jicho kwa kweli! (Moyo wangu viraka, niloshonea ni vingi Yanauchana mashaka, usaliti ulo mwingi) Angakukosea mtu, mawi yasostahili, Usimkosee utu, ufanye kumkejeli, Umwone kama kiatu, za chooni champali. (Moyo wangu viraka, niloshonea ni vingi Yanauchana mashaka, usaliti ulo mwingi) Asilie ukicheka, uone umemuweza, Wasaa aungulika, uzidi na kumbeza, Moyo wangu viraka, niloshonea ni vingi Yanauchana mashaka, usaliti ulo mwingi Amalizapo kulia, utakuwa ndio mwanzo, Kilio nawe kutoa, katika mwanzo wa funzo. Moyo wangu viraka, niloshonea ni vingi Yanauchana mashaka, usaliti ulo mwingi Moyo, Rehani ulotobolewa, matundu kulemewa, Takosa pa kushonewa, afua kununuliwa, Gharama yake elewa, bila shaka kung’olewa! Hatima yake? Moyo wangu viraka, niloshonea ni vingi Yanauchana mashaka, usaliti ulo mwingi Malenga wa Vilimani Kelvin Kombo Motuka Disemba 27, 2024