
ADHAMA YA MTU Kitaka lolote jambo, chudi utalifanyia, Si kupigana vikumbo, kwa nguvu kujipatia, Jua adhama ya mtu, hutoka kwake mwenyewe. (Mla chake hana haya, siye mfata mwairo Tamaa mbele walisema, nyuma yaja mbio mauko) Lingakusuma tumbo, kwa wivi kulifikia, Bora liimbie wimbo, kwa saburi kutulia, Jua adhama ya mtu, hutoka kwake mwenyewe. (Mla chake hana haya, siye mfata mwairo Tamaa mbele walisema, nyuma yaja mbio mauko) Unayataka mapambo, ya wajihi nazo pua, Si wa lazima urembo, wa kudoea rubaa, Jua adhama ya mtu, hutoka kwake mwenyewe. (Mla chake hana haya, siye mfata mwairo Tamaa mbele walisema, nyuma yaja mbio mauko) Malenga wa Vilimani (Kelvin Kombo Motuka) Novemba 30, 2024

